Kuhusu Union

Kuhusu NTUC

Union ya Kaskazini mwa Tanzania (NTUC) ni sehemu ya Kanisa la Waadventista wa Sabato duniani, chini ya Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati. Makao makuu ya Union yako Njiro, Arusha. Eneo lake linaanzia Tanga upande wa mashariki hadi Kigoma upande wa magharibi, na linajumuisha sehemu za Kanda ya Ziwa.

Union inaratibu kazi ya utume, inasaidia uongozi wa Kanisa na kushirikiana na taasisi za Waadventista. Konferensi na fildi zinasimamia wachungaji, makanisa na huduma za Kanisa katika maeneo yao.

Utume wetu

Utume wetu ni kuwafanya watu wote kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo, kutangaza Injili ya milele katika muktadha wa Ujumbe wa Malaika Watatu, na kuuandaa ulimwengu kwa marejeo ya Kristo yaliyo karibu. Tunatekeleza utume huu kwa kufundisha Biblia, kufanya wanafunzi, kuhubiri, kuponya na kuhudumia.

Mathayo 28:18–20 · Matendo 1:8 · Ufunuo 14:6–12

Njozi yetu

Tunatazamia utume wetu kufikia kilele katika mpango wa Mungu wa kuurejesha uumbaji wake katika ukamilifu wa mapenzi na haki yake.