Historia Yetu

Historia yetu

Kazi ya Waadventista wa Sabato nchini Tanzania ilianza mwaka 1903, wakati Abraham C. Enns na Johannes Ehlers walipowasili Tanganyika na kuanza kazi miongoni mwa jamii ya Wapare. Jengo la kwanza la kanisa la Waadventista wa Sabato nchini Tanzania lilijengwa Giti Miamba, katika Milima ya Pare.

Kanisa lilipoendelea kukua, Tanzania Union Mission iligawanywa kuwa Union mbili. Union ya Kaskazini mwa Tanzania iliundwa Desemba 2013, ikiwa na makao makuu Arusha. Konferensi Kuu ya Kanisa ilizitambua rasmi Union hizo mbili mwaka 2015.

Mwaka 2025 ziliundwa fildi za North Mara, North-West Tanzania na Simiyu River. Mkutano Mkuu wa Nne wa Union ulifanyika Septemba mwaka huo katika Chuo Kikuu cha Arusha.